Jumamosi , 12th Sep , 2020

Mgombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amedai kuwa katika uongozi wake wa miaka mitano akiwa kama Mbunge wa jimbo kuna ahadi alishindwa kutekeleza.

Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe

Zitto ametoa kauli hiyo wakati akizindua kampeni yake ambapo alikiri kuwa kuna ahadi zilishindwa kutimizwa ikiwemo kuishawishi Manispaa ya mji huo kuinunua timu ya Mashujaa ili Mkoa huo upate timu itakayowawakilisha Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

"CCM ilitukwamisha tulitaka kuishawishi manispaa ili kuinunua timu ya Mashujaa ili tupate wawakilishi wa Mkoa katika mchezo wa soka Ligi Kuu, lakini tutaendelee kupambana ili tupate timu kutoka Kigoma itakayopanda kucheza Ligi Kuu", amesema Zitto.

Zitto ameongeza kuwa, "Katika kipindi cha miaka 5 nimefanya kazi kubwa kushirikiana na wabunge wengine wa mkoa wa Kigoma kupaza sauti ili barabara za mkoa wa Kigoma zijengwe kwa lami kama ilivyo mikoa mingine hapa Tanzania".