Ijumaa , 29th Mei , 2020

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, imemuachia huru Kiongozi wa Chama cha ACT azalendo, Zitto Kabwe kwa sharti la kwamba, asitoe matamshi ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Kesi hiyo ya uchochezi namba 327 ya mwaka 2018, Zitto alikuwa anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28, 2018, wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho.

Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa kuwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari alitoa naneno ya uchochezi yenye nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi.

Ilidaiwa kuwa Zitto Kabwe alizungumzia mauaji, yaliyotokea katika Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza mkoani Kigoma ambayo yalisababishwa na vurugu kati ya Polisi na raia.

Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza Zitto Kabwe, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 2, 2018,