Alhamisi , 23rd Jan , 2020

Rais Dkt. John Magufuli amemteuwa Mbunge wa Ilala Dar es salaam Mh. Mussa Azzan Zungu kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira.

Kutoka kushoto ni Mussa Azzan Zungu, Kangi Lugola na George Simbachawene

Rais pia amemteuwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Simbachawene anachukua nafasi ya Kangi Lugola, ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo Januari 23, 2020 na Rais Magufuli kwa kile alichoeleza kutoridhishwa na utendaji kazi katika Wizara hiyo.

Aidha Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali Jacob Kingu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi leo Jenerali Kingu alikuwa Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani mpaka jana Januari 22,2020 ambapo aliandika barua ya kujuizulu nafasi hiyo na Rais akakubali ombi lake.