Askofu Maluma kuzikwa kesho

Jumatatu , 12th Apr , 2021

Mwili wa aliyekuwa Mhashamu Baba  Askofu wa Jimbo katoliki la Njombe Alfred Maluma  umewasili leo katika uwanja wa ndege wa Mkoa wa Njombe na kupokelewa na Maelfu ya waombolezaji.

Mwili wa aliyekuwa Mhashamu baba  askofu wa Jimbo katoliki la Njombe Alfred Maluma ulipowasili uwanja wa ndege wa Njombe

Askofu Maluma alikutwa na umauti April 6 katika Hospitali ya taifa ya Mhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali.

Mwili wake unatarajiwa kupumzishwa katika nyumba yake ya milele hapo kesho aprili 13 katika makaburi maalumu yaliyopo ndani ya kanisa kuu la mtakatifu Yosefu alipo kuwa akihudumu wakati wa uhai wake.