Jumatatu , 15th Feb , 2021

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeombwa  kutoa elimu ya mlipa Kodi kwa wafanyabiashara ili kupunguza changamoto zilizopelekea zaidi ya biashara 600 kufungwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Baadhi ya wafanyabiashara walioudhuria semina ya elimu ya mlipa kodi iliyokuwa inaendeshwa na TRA , mkoani Geita.

Ombi hilo limetolewa na baadhi ya wafanyabiashara mkoani Geita wakati wa semina ya elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara na waandishi wa habari iliyokuwa inaendeshwa na mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa wakili Renatus Malecha amesema kama wananchi wangejua kiasi gani cha kodi wanatakiwa kulipa ingeweza kuwasaidia watu wasiwe wanafunga maduka kwani  kutotoa elimu ndio sababu ya wananchi wengi washindwe kulipa kodi kwa wakati na mara wasipolipa wanotozwa faini na TRA ambayo hounekanana kama kodi.

Aidha Kwa upande wa Meneja wa TRA katika mkoa huo Hashim Ngoda ameeleza sababu iliyopelekewa biashara hizo kufungwa"Biashara zilizofungwa mkoani Geita zipo kama mia sita na sitini hivi kwa mwaka 2020, lakini katika biashara hizo zilizofungwa hakuna hata biashara moja ambayo sababu ya kufungwa kwake ilikuwa ni kodi, waliokuwa na changamoto za kodi tumekuwa tukiongea nao, biashara hizo hazikufungwa kwasababu ya kodi bali kwasababu mbalimbali ambazo zimekuwa zinaandikwa kwenye barua zao" amesema Hashim Ngoda