Jumamosi , 20th Apr , 2019

Mwanamuziki wa kike wa hip hop bongo Frida Amani au Queen Fifi, ametaka wanaume kutomuogopa kutokana na muonekano wake, na wamtongoze kama wafanyavyo kwa wengine.

Frida ametoa kauli hiyo kwenye Friday Night Live inayorushwa na East Africa Television alipokuwa akiachia video ya wimbo wake mpya wa 'Pull up', na kusema kwmaba yeye ni mtu wa kawaida na anapendwa na wengi sana.

Frida afunguka

 

'Unajua wapo walionitongoza na probably walinipata, jamani mimi ni mtu wa watu, na mnitongoze jamani”, alisikika Frida Amani.

Hapo jana Frida Amani amechia kazi yake mpya inayoitwa Pull up akimshirikisha Gifted Son, ambayo mwenyewe amesema ni moja ya kazi ambazo zinakuja kuwapoteza wasanii wengine wa hip hop kutokana na ubora wa hali yajuu.

Mwanamuziki Frida Amani