Ijumaa , 17th Aug , 2018

Familia ya msanii wa miondoko ya bongo fleva na Taarabu Hammer Q, imepata pigo kwa kufiwa na ndugu wanne wa familia moja kwa wakati mmoja, katika ajali ya boti binafsi waliyokuwa wakisafiria kutoka Zanzibar kuelekea mkoani Tanga.

Familia ya msanii wa miondoko ya bongo fleva na Taarabu Hammer Q

ayo yamebainishwa na muimbaji huyo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram na kudai ajali hiyo imetokea siku tatu za hivi karibuni ambapo asubuhi ya leo wamebahatika kuupata mwili wa baba yake kando kando ya fukwe huko Pangani mkoani Tanga.

"Alhamdulilah mwili wa marehemu baba yangu umeokotwa pangani Tanga, muda wowote utasafirishwa kwa ajili ya kuja kuhifadhi katika nyumba yake ya milele", ameandika Hammer Q.

Aidha, Hammer Q kabla ya kutoa taarifa hiyo ya kupatikana kwa mwili wa baba yake, asubuhi ya leo amesema kwamba walikuwa wakiutafuta mwili wa baba yake kwa takribani siku ya tatu leo baada ya kupotea majini.

Akizungumza na www.eatv.tv Hammer Q amesema katika tukio la kuokotwa kwa baba yake lakini pia ilipatikana miili mingine miwili ya ndugu zake hao na kufanya jumla ya miili minne ya ndugu zake wote  kupatikana huku mmoja ukiwa tayari umeshazikwa.

Aidha amesema kuwa baada ya kuwasili miili hiyo taratibu za mazishi zitafuta kwa mujibu wa sheria na makubaliano ya familia.

Msikilize hapa chini Hammer Q akielezea tukio zima jinsi lilivyokuwa