Jumanne , 9th Feb , 2021

Mpenzi wa zamani wa Wema Sepetu Patrick Christopher ambaye anadaiwa kumtapeli zaidi ya milioni 60 staa huyo wa filamu amefunguka kusema, Wema Sepetu ni mwanamke ambaye haijui 'future' yake na anapenda sana starehe.

Kushoto ni Wema Sepetu na aliyekuwa mpenzi Patrick Christopher

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Patrick Christopher amesema alikuwa kwenye mahusiano na Wema Sepetu kwa kipindi cha miaka mitatu ila waliamua kuachana baada ya kuvuja kwa video zikiwaonesha wakiwa faragha.

"Tulikaa kwenye mahusiano karibia miaka mitatu, yupo tofauti ni wanawake wengine wanaojituma yeye haijui 'future' yake, anaishi kwa kuangalia leo tu na mpenda starehe, tulifikia hatua ya kuachana kwa sababu alikuwa ana-post vitu vya ajabu wakati mimi nina mtoto mkubwa na viliniletea aibu kwenye jamii" amesema Patrick Christopher

Zaidi mtazame hapo chini kwenye video.