Jumatano , 23rd Oct , 2019

Video Vixen aliyejipatia umaarufu mitandaoni Amber Rutty ameieleza EATV & EA Radio Digital kuwa ana ndoto za kumiliki timu ya mpira kupitia watoto ambao atajaliwa kuwapata yeye na mume wake Davil.

Amber Rutty

Amber Rutty amesema mpaka sasa yeye na mumewe wamefikisha mwaka mmoja wa ndoa yao ila hapo awali walikuwa kwenye mahusiano kwa miaka 6, ila mipango ya kupata watoto wamemuachia Mungu.

"Mtoto ni majaliwa ya Mungu kwa sababu ndiyo anabariki, sisi binadamu hatuwezi kusema tunataka watoto, na ingekuwa inawezekana basi tungekuwa tunataka vitu fulani na tunavipata  kama ni hivyo watu tungekuwa tumeshazaa sana ila tukibarikiwa mtaona watoto wetu" ameeleza Amber Rutty.

"Mimi nimepanga kuwa na watoto 11 yaani timu ya mpira kwa sababu nina mipango ya kuzaa watoto hao ili kutengeneza timu ya mpira ili wanangu wawe wachezaji, ila bado sijajua nitawapa jina gani" amenongeza.

Aidha  Amber Rutty amesema yeye ni muislam kamili na anaijua dini vizuri pia ana mipango ya kusomea kila kitu kuanzia lugha ya Kiingereza hadi Kihindi kwa sababu anaogopa kufeli katika maisha.