Amber Rutty ataka kuongea na Rais wa Marekani

Jumatatu , 6th Jan , 2020

Video Vixen na msanii Amber Rutty, amesema ameanza kujifunza lugha ya Kiingereza ili siku moja aje kuongea na Rais wa Marekani, Donald Trump, pamoja na kuwa na uwezo wa kuongea na mtu yeyote yule asiyejua Kiswahili.

Video Vixen, Amber Rutty.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Amber Rutty amesema ni kweli hajui kuzungumza lugha ya Kiingereza ila kwa sasa yupo shuleni kujifunza lugha hiyo.

"Nipo shule nasomea lugha ya Kiingereza ili niweze kufika mbali kuongea na mtu yeyote ambaye hajui Kiswahili, pengine hao wanaoni diss sijui Kiingereza hata kusema neno I love you hawajui, ila mimi nasoma hata Kiingereza cha maji hivyo hivyo naongea" amesema Amber Rutty.

Aidha Amber Rutty  ameongeza "Naendelea kusoma kwa sababu mimi ni msanii naweza kufika nchi mbalimbali ambazo watu hawazungumzi Kiswahili, au naweza kupata bahati ya kwenda Marekani nikapewa Rais wao niongee naye, kama sitajua kiingereza nitakosa bahati hiyo"