Jumatano , 22nd Jan , 2020

Kamera za EATV & EA Radio Digital, zimekutana na msanii kutokea visiwani Zanzibar AT, ambaye amesema akikutana na Chris Brown kwenye Mmoja, hakuna atakayemfunika mwenziye.

kulia pichani ni AT, kushoto ni Davido

AT amesema hatamuachia Chris Brown amtawale kwenye wimbo kama alivyomfanyia Davido, kwenye wimbo wa blow my mind, ambapo staa huyo wa Marekani alipiga vibao kutokana na ufundi wake.

"Nilichojifunza kwenye wimbo wa blow my mind ya Davido na Chris Brown ni mwanamuziki amefanya wimbo na msanii, nimeona jinsi jamaa alivyopigwa vibao na kipigo kile atawaambia Waafrika wote kwamba, hawa watu sio wazuri, Chris Brown ameimba kwa kutumia ufundi alimchanganya sana Davido na nimepata elimu" amesema AT. 

Aidha ameongeza kusema "Vyovyote utakavyofanya ukikutana na Chris Brown, kwenye wimbo mmoja lazima atakupiga, kama  nikifanya naye tutakachotofautiana labda ni lugha tu yeye ataimba Kiingereza mimi Kiswahili, yule jamaa sio mdogo lakini kunifunika sio rahisi na kumfunika ni kazi kitakachotokea ni bila bila".