Audio: Mapenz* yamponza Baraka The Prince

Wednesday , 13th Sep , 2017

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Baraka The Prince kwa mara ya kwanza amefunguka sababu ya kuondoka kwenye uongozi ulioanza kumsimamia kazi zake na kumtambulisha kwenye game Tetemesha Records, ambayo imemgharimu mpaka sasa.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Baraka amesema sababu kubwa iliyomtoa Tetemesha ni mahusiano ya kimapenzi na msanii wa filamu ambaye uongozi huo hawakutaka awe naye.

Akiendelea kupiga stori na Big Chawa Baraka The Prince amesema kwamba kwa sasa hawezi kumtaja muigizaji huyo, walisafiri na mpenzi wake huyo na baada ya uongozi kusikia taarifa hiyo, waliamua kumsimamisha kazi, na alipojaribu kukaa nao chini kuzungumza hawakumuelewa.

Msikilize hapa chini akipiga stori na Big Chawa