Audio: Natetea penzi la Eddy Kenzo - Saida Karoli

Monday , 11th Sep , 2017

Msanii wa muziki ambaye ni mkongwe kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania Saida Karoli, amesema sababu ya kufanya kolabo na msanii Eddy Kenzo wa Uganda ni kutokana na upendo wa msanii huyo juu yake

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Saida Karoli amesema Eddy Kenzo ana mapenzi makubwa kwake, hivyo akaona ni vyema atetee upendo wake huo kwa kufanya naye kazi.

Pia Saida Karoli amesema kwa sasa msanii huyo ndiye anayekubalika zaidi Afrika Mashariki kutoka nchini Uganda, hivyo ni wakati muafaka kwake kujaribu kupenya zaidi kwa kumtumia Eddy Kenzo.

Hivi karibuni Saida Karoli amefanya kolabo na wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa kiume Belle 9 na G nako, na kazi hiyo kufanya vizuri kwa muda mfupi.

Msikilize hapa chini