"Baba Levo ni shetani"-Peter Msechu

Jumamosi , 8th Feb , 2020

Msanii Peter Msechu amemwabia rafiki yake Baba Levo kuwa ni shetani kwa sababu anamiliki wanawake wengi na kila mwanamke amepata naye mtoto, kwa hiyo anamtaka atulie na ajifunzie kupitia yeye.

Picha ya pamoja ya Wasanii Peter Msechu na Baba Levo

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Peter Msechu amesema Baba Levo hawezi kupata neema za Mungu hadi achague mwanamke mmoja wa kuishi naye, kutulia  na kufunga naye ndoa.

"Baba Levo lazima aelewe maisha ni gharama sana najua kufunga ndoa hawezi kama pete ina thamani ya Milioni 4 au 5, tabia yake ya kucheza kamari ataiotolea wapi, na baraka lazima upewe na Mungu halafu yeye ni shetani ana wanawake wengi hawezi kutoboa kwa sababu hajui chaguo lake" amesema Peter Msechu 

Aidha Peter Msechu ameendelea kusema "Kila mwanamke anayekutana naye anazaa naye, mwambieni aendelee kuzaa atachagua kisha kumpata  mwanamke mzuri ambaye atamvumilia  lakini  sidhani  kama atafanikiwa ila aendelee kujifunza kupitia sisi wakongwe" ameongeza 

Msanii huyo amefunga ndoa siku za hivi karibuni na mke wake Amariss Lauren siku kadhaa zilizopita.