Jumamosi , 19th Oct , 2019

Rapa Country Boy, amesema bata na starehe alizokula Young Dee nchini Marekani, limeshaisha na amekiri amewakomesha wasanii wenziye kwa vitu alivyokuwa anafanya kipindi yupo nchini humo kwa kutumia picha ambazo alikuwa anaweka katika mtandao wa Instagram.

Msanii Young Dee

Country Boy amesema hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kutoa maoni yake kuhusu maisha ya Young Dee nchini Marekani, baada ya kuondoka Tanzania mwezi wa nne mwishoni mwaka huu,

''Bata limeisha nadhani yupo njiani lakini amejitahidi na ametukomesha vizuri sana akirudi tunachotaka kukiona ni kazi. Mimi siamini sana kwenye kula bata au starehe, huwa nataka vitu kama hivyo viende na kazi zake, kama ameweza kufurahia na kutulia nadhani atakuwa Young Dee mpya halafu namuamini ni mmoja kati ya wanyamwezi ambao wana swaga sana ila nataka kuona kazi zaidi" ameeleza Country Boy.

Pia amesema hata yeye ni mmoja wa wasanii ambao wameshasafiri sana kwenda nchi za nje kama Afrika Kusini, Ujerumani, nchi za ukanda wa Afrika Mashariki pia ana safari nyingine mwishoni mwa mwaka huu kwenda Ujerumani kwa hiyo hashtuki akiona wasanii wanavyosafiri kwa sababu tayari ameshapata huo uzoefu.