Ben Pol ampa ujumbe mzito Ebitoke

Monday , 16th Oct , 2017

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ilikuwa inasemekana yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji wa vichekesho Ebitoke, amemtaka msanii huyo kuwa na subira juu ya yale anayoona anamkosea na kusema muda utafka na kila kitu kitakuwa sawa.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ben Pol amesema anaamini mpenzi wake huyo anaelewa mazingira ya kazi zake jinsi yalivyo, na mchaka mchaka wa ubize ambao alikuwa nao kwenye kazi zake za muziki.

"Mimi naamini anaelewa, saa nyingine uko safarini hakuna mtandao, nafikiri tuwe na subira vitu vingine vingi tutapata ufumbuzi wa kila kitu, unajua kila mtu ana mapungufu yake, unaweza ukakosea sehemu baadaye mkaelewana mkasahau", amesema Ben Pol.

Hivi karibuni Ebitoke alisikika akisema kuwa Ben Pol hapokei simu zake wala hajibu message zake, na kuomba watu wamsaidie kumuuliza Ben Pol amekutwa na nini mpaka kufikia hatua hiyo.