Jumapili , 17th Nov , 2019

Mhamasishaji wa timu ya taifa Nicky Bongozozo, amemuomba msamaha Mke wake Caro Jessica, kwa kosa lake la kuongea kwa kupitiliza, hali iliyopelekea mkewe huyo kufuatwa na kutukanwa na watu mitandaoni.

Mhamasishaji wa timu ya taifa Nicky Bongozozo.

Kupitia mitandao yake ya kijamii wa Instagram na Twitter  wa Nicky Bongozozo ameandika kuwa "mama Jessica wangu nakupenda sana kwa zaidi ya miaka 20 na upendo wangu utakuwepo mpaka siku yangu ya mwisho, naomba msamaha kwa makosa yangu yote hasa kuropoka ropoka ovyo, Nilikosea ilibidi niweke maisha yetu "private" nisitangaze kwa watu millioni 30"

"Sijaridhika kabisa unavyoniambia watu wanakufuata "inbox" wanakutukana na kukuonea. suala la uonevu kwenye mtandao ni kubwa ila watu wajue wakionea familia yangu wamenionea mimi, mwendo wangu ni kujaribu kufurahisha watu si kuongelea Taifa Stars tu" ameandika Bongozozo

"Najitahidi kutoa burudani upande wa muziki, vituko, kucheza, na clips nyingine zinazoleta raha kama naona mama watoto wangu anaonewa, nitaacha kutoa hizo kumbukeni moyo si chuma, maneno mengine yanauma" ameongeza

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Mama Jessica wangu @carojessica3, nakupenda sana kwa zaidi ya miaka 20 na upendo wangu utakuwepo mpaka siku yangu ya mwisho. . Naomba msamaha kwa makosa yangu yote hasa kuropoka ropoka ovyo. Hii kazi ya kuwa mtu maarufu mimi mgeni na mshamba sana, tena wa kijijini ndaaaani, basi kuongelea sisi tunavyoishi nilikosea. Ilibidi niweke maisha yetu private nisitangaze kwa watu millioni 30 . . Sijaridhika kabisa unavyoniambia watu wanakufata inbox wanakutukana na kukuonea. Suala la bullying(uonevu) kwenye mtandao ni kubwa kumbe ila watu wajue wakionea familia yangu, wamenionea mimi. . Mwendo wangu ni kujaribu kufurahisha watu si kuongelea Taifa Stars tu. Najitahidi kutoa burudani upande wa muziki, vituko, kucheza, na clips nyingine zinazoleta raha. Kama naona mama watoto wangu anaonewa, nitaacha kutoa hizo burudani nyingine. Mtasikia mambo ya mpira tu. Au mtaona kimya kabisa. No more Bongozozo. . Jamani kumbukeni: Moyo si chuma, maneno mengine yanauma. . #bongozozo #fujoisiyoumiza

A post shared by Bongozozo (@bongozozo_tanzania) on

Nicky Bongozozo amejipatia umaarufu kupitia mtandao wa Instagram, baada ya kuwa anaongea Kiswahili fasaha hali ya kuwa yeye sio mtanzania, huku akiishabikia timu ya Tanzania, kwenye mashindano ya Kombe la Afrika "AFCON" yaliyofanyika mwezi Juni hadi Julai mwaka 2019.