Alhamisi , 10th Jun , 2021

Hatimaye msanii Burna Boy wa Nigeria amepokea Tuzo (Plaque) yake ya Grammy aliyoshinda Machi 16, 2020 katika msimu 63 wa tuzo hizo kupitia kipengele cha “Best Global Music Album” kupitia album yake ya “Twice as Tall”.

Picha msanii Burna Boy

Burna ame-share picha na video mbalimbali za uthibitisho wa kupokea Tuzo hiyo kwenye mtandao wa instagram mapema leo na kuacha ujumbe unaoashiria ni kiasi gani ana furaha na kumshukuru Mungu.

Gwiji huyo maarufu wa Afrika ndiye mshindi wa kwanza wa tuzo ya Afrobeat  kutoka Nigeria.