Alichogundua Mabeste baada ya kusalitiwa na mkewe

Ijumaa , 17th Jan , 2020

Msanii wa HipHop Mabeste, amefunguka kwa kusema kati ya vitu vilivyosababisha aachane na aliyekuwa mke wake na mzazi mwenziye ni kumsaliti kwa kutembea na rafiki yake pamoja na kutokuwa na pesa.

Picha ya Mabeste akiwa na mkewe Lisa, enzi za mahusiano yao

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Mabeste amesema kuwa mzazi mwenziye ndiyo aliyeanza kumwambia kwamba waachane, jambo ambalo limemuumiza sana.

"Mimi na yeye tulikata hizo stori tangu mwaka jana, tulikuwa hatuongei na hata watoto hajawahi kuniletea niwaone nikimtumia ujumbe kuhusu familia yangu hanijibu, alinifata akaniambia tuachane nikakubali, mtu ambaye ameenda kuishi naye ni rafiki yangu ambaye tunafanya kazi" amesema Mabeste.

Aidha Mabeste ameendelea kusema "Siwezi kumtaja huyo rafiki yangu anayeishi naye kwa sasa ila ni muongozaji wa video 'Director', nilikuwa namuuliza kitu gani kinaendelea anakataa, mke wangu nilimpa uhuru sana, kumbe alikuwa akitoka Moshi kuja Dar analala kwa jamaa, mimi ananidanganya kwamba yupo kwa dada yake" ameongeza.

Cha mwisho amesema alichokigundua hadi imesababisha kuachana kwao  ni kuyokuwa na pesa za kutosha.