
Msanii Chemical
Chemical amepata 'Scholarship' hiyo baada ya ku-graduate na kupewa tuzo ya kuwa mwanafunzi mwenye tafiti bora (first winner) wa Chuo kizima kwa mwaka 2021/22 katika Chuo cha UDSM.
"Project yangu nilikuwa nafanya kitu ninachokipenda, nilifanyia tafiti nyimbo zinazoimbwa na wavuvi ambavyo mtu akisikia anaweza akachukulia poa lakini ikashindanishwa na idara mbalimbali Chuoni lakini yangu ikawa bora" ameeleza Chemical
Mwana wa Lubao mwenyewe ametusanua kwamba amepata Scholarship ya kuendelea na PHD katika Chuo Kikuu Cha St Andrew's ambacho amesoma Mwana wa Mfalme Prince William kilichopo huko Scotland.