Dogo Janja apiga goti kwa Linna

Jumatatu , 10th Feb , 2020

Msanii Dogo Janja ameonekana kupiga goti na kumvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa sasa ambaye ni mfanyabiashara kutoka mkoani Arusha aitwaye Linnahonnah maarufu kama "Quenlinnatotoo".

Picha ya msanii Dojo Janja

Taarifa hiyo imekuja baada ya kupostiwa kwa kipande cha video fupi katika ukurasa wa mtandao wa Instagram wa msanii Linah Sanga, ambayo inaonyesha Dogo Janja akipiga goti kwenye boti na kumvalisha pete mchumba wake huyo.

Kupitia video hiyo Linah Sanga ameandika kwa kumpongeza Dogo Janja baada ya kufanikisha kufanya tendo hilo kwa mpenzi wake.

Madee, Linah na Recho ni baadhi ya wasanii ambao wameenda visiwani Zanzibar kula bata pamoja na kusheherekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mpenzi huyo wa Dogo Janja.

Kabla ya kuwa kwenye mahusiano na Quenlinnatotoo Dogo Janja alikuwa kwenye ndoa na msanii wa filamu Irene Uwoya, pia amekuwa msanii wa kwanza kumvalisha pete mpenzi w

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

She said “YES” Congrats @dogojanjatz @quenlinnatotoo

A post shared by Linah Sanga (@officiallinah) on

ake huyo kwa mwaka 2020.