Dogo janja amekuwa James delicious ?- Young Tusso

Ijumaa , 16th Mar , 2018

Msanii wa HipHop nchini Tanzania, Young Tusso amefunguka na kumtaka Dogo Janja aende kuwaomba radhi wananchi wa mkoa wa Arusha kwa madai amewakosea sana kwa kitendo chake cha yeye kujifanya mwanamke katika video yake mpya ya Wayuwayu.

Young Tuso ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea Janjaro kutoa video ya wimbo huo na kupelekea kupondwa kwa watu wengi kwa kitendo alichokionesha licha ya kuwa wimbo huo mpaka sasa kuonekana kupendwa.

"Nilistushwa sana baada kuona instagram picha za Dogo Janja kumuona amekuwa mwanamke maana hata hivyo video haikuwa na ulazima wa weye kuwa mwanamke kwa hiyo mimi nimemtazama kama mtoto wa kiislamu. Dogo Janja sasa inabidi akaiombe msamaha Arusha", amesema Young Tusso.

Pamoja na hayo, Young Tusso ameendelea kwa kusema "nafikili mimi nipo tofauti kidogo sikubaliani na yeye kuwa 'video vixen'. Unajua kumuona msanii kama Dogo Janja halafu wa HipHop ambaye anatokea Arusha wenye asili ya ugumu kidogo kwa hiyo mwisho wa siku unamuona amekuwa James delicious tena inanipa tabu sana kuona hivyo"

Mtazame hapa chini Young Tusso akiendelea kufunguka zaidi.