Dorah ajibu madai ya kudate na KibenTen

Jumapili , 6th Oct , 2019

Muigizaji wa Tamthilia hapa nchini ajulikanaye kwa jina la Dorah,amesema kuwa mwanaume aliyekuwa naye kwa sasa kwenye mahusiano amemzidi kiumri, ambapo mpenzi wake huyo ana miaka 23, huku yeye akiwa na umri wa miaka 2.

Dorah ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachoruka kila siku ya Jumatano kupitia kurasa za Facebook na Youtube za East Africa TV, na kumtaja jina la Edson ambaye kwa sasa bado ni mwanafunzi wa chuo.

"Kwa sasa mpenzi wangu anamiaka 23 na mimi nina miaka 24 na nilianza naye nilipokuwa nimemaliza kidato cha nne, kifupi huyu ni mpenzi wangu wa kwanza, na mtu akisema nambemenda atakuwa ameamua yeye tu kusema" amesema Dorah.

Aidha Dirah ameongeza kuwa,"kingine kwa sasa anasoma Iringa, mwingine akisema mimi natoka na Kibenten bado simkatazi, kwa sababu atakuwa ameamua yeye"

Tazama mahojiano kamili