Alhamisi , 22nd Mar , 2018

Msanii wa filamu na mchekeshaji hapa bongo Ebitoke, ameweka wazi juu ya kufufuka kwa penzi lake na Ben Pol ambaye hapo awali alidai hapokei hata simu zake, na hivi karibuni kuanza kuwa pamoja tena.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Ebitoke amesema kwamba kitendo cha yeye kuonekana na Ben Pol kwenye kazi zake za comedy ni kwamba alishamuahidi kuwa atamsaidia kwenye kazi zake, na si ndumba kama baadhi ya watu wanavyodai, kutokana kwamba penzi lao lilishakufa.

“Sijamroga Ben Pol, hata hivyo kipindi cha kati kati ambacho mahusiano yetu hayakuwa sawa, sio kwamba hayakuwa sawa ni kwamba alinituliza nisiongee sana kwenye mitandao baada ya ile kusema hapokei simu zangu na kuwa niweze ku-manage mahusiano, tulikaa kama mwezi mzima tulikuwa hatuongelei chochote, lakini aliniahidi kuwa atanisaidia kazi ndo hivyo tunasaidiana”, amesema Ebitoke.

Wawili hao bado kuna sintofahamu kama ni kweli wapenzi, kwani mara nyingi Ben Pol amekuwa sio mtu wa kufurahia suala la mahusiano yake na Ebitoke kuwa wazi.