Enock Bella avunja ukimya

Wednesday , 13th Sep , 2017

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alikuwa katika kundi la Yamoto Band, Enock Bella, ameamua kuwajibu wanaomdharau kuwa hajui kuimba kwa kuwa yuko kimya kuliko wenzake wote wa Yamoto Band, kwa kuachia kazi yake mpya hivi karibuni.

Enock Bella

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Enock Bella amesema si kama hajui kuimba, bali uongozi ulikuwa na wasi wasi naye, lakini pia imekuwa na faida kwake kwani alitumia muda huo kutafuta 'conection' na wasanii wa nje ya Tanzania, na kuwataka mashabiki kukaa tayari kwa kolabo zake na wasanii hao.

"Kukaa kimya kote kuna mipango, ukimya wangu mimi ulikuwa unatengeneza mipango, ukimya ule pia umesababisha conenction na nje, nimefanya collabo za nje, pia uongozi ulikuwa tatizo kwa sababu ilikuwa ni ngumu mtu kuweza kumchukua Enock Bella kufanya nye kazi kwa sababu kwenye Yamoto nilikuwa naimba vipande vidogo vidogo, kwa hiyo mtu lazima upate mashaka, lakini sasa hivi uongozi uko sawa na natarajia kuachia kazi yangu mwezi huu wa 9", alisema Enock Bella.

Enock Bella ni miongoni mwa wasanii waliokuwa Yamoto Band, lakini hajaachia kazi yoyote mpaka sasa, huku wenzake wawili Beka Flevour na Aslay  wakiwa na kazi sokoni.