Enock Bella kuhusu kiny'ongo kwa wenzake wa Yamoto

Ijumaa , 14th Sep , 2018

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Enock Bella amesema hajisikii wivu wa aina yoyote kuwaona ndugu zake waliokuwa kwenye kundi moja la Yamoto Band, kufanikiwa kimuziki kwa madai laiti na yeye angekuwa na mtu nyuma yake basi wasingeweza kumfikia kimafinikio hata kidogo.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Enock Bella

Enock Bella amebainisha hayo alipokuwa anapiga stori na www.eatv.tv na kusema kuwa sababu kubwa ya yeye kutokuwa na wivu na wakina Aslay, Beka Flavour pamoja na Maromboso ni kutokana hawapambani wao kama wao.

"Siwezi kujisikia wivu kutokana na mafanikio ya wenzangu waliyo kuwa nayo hadi hii leo, kwasababu wao wanafanya muziki kwa kusukumwa na mtu nyuma yao, bibi sina hao watu na badala yake ninatumia nguvu ya umma katika kukamilisha mambo yangu", amesema Enock Bella.

Pamoja na hayo, Enock Bella ameendelea kwa kusema kuwa "laiti ningekuwa na watu nyuma yangu wanahakikisha muziki wangu unaenda, siwafichi mimi ningekuwa mtu ambaye sifanani na yoyote kwa wasanii tuliotoka Yamoto Band, maana nina hazina kubwa ya kazi zangu".

Enock Bella ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wanavutiwa na wengi wakati walipokuwa katika kundi la Yamoto Band kutokana na uzuri wa sauti yake ya 'base' lakini lilipokuja kuvunjika kundi hilo, ili mchukua muda mrefu hadi alipokuja kutoa kazi yake ya awali lakini hakuweza kupata mapokezi mazuri.