
Fid Q amefunguka hayo leo akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo, East Africa Radio wakati akieleza kwa nini wimbo wake mpya wa 'Ulimi Mbili' ameuachia pasipo kuufanyia 'mixing'.
"Majani alikuwa amelazwa hivyo kufanya 'mixing' ikawa shida kidogo na mimi sikutaka kumkalia kooni kwani najua akipata nafuu tutaumalizia na video yake tutaitoa kabisa. Sijataka kwenda kwa prodyuza mwingine kufanya kazi hii kwani kwa sikio la Majani jinsi linavyoujua muziki nisingeweza kumpa mtu mwingine kazi ya mpishi huyu" Fid alifunguka
"Lakini ujue hii kazi pamoja na kwamba ipo 'rough' haijafanyiwa 'mixing' kwa studio zingine nyingi hapa bongo hapo ndo ungekuwa umekamilika. Sitaki kuzikosea heshima studio zingine lakini kwa bongo Majani hana mfano. Maproduza wengi wakali kuliko majani wapo lakini hawajui kufanya 'mixing'" aliongeza Fid
Hata hivyo wawili hao wamekuwa na muungano mzuri kwa kipindi kirefu hali ambayo huwa inamfanya produza Majani aseme rapa Fid Q ni rapa wake bora ulimwenguni naye Fid Q kusema Majani ni mtayarishaji wa muziki levo za kimataifa.