Jumatano , 20th Feb , 2019

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Songa ameeleza juu ya mipango yake ya harusi itakavyokuwa huku akiahidi chakula hadi kwa mifugo itakayohudhuria.

Baadhi ya wasanii wakongwe wa Hip Hop ambao wameoa

Songa ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema hawezi kukubali watu waondoke na chakula katika siku ya harusi yake.

 

Msanii huyo alifahamika na wengi alipoachia wimbo wake wa 'Mwendo tu' aliomshirikisha Jay Moe, wimbo ambao ulitoka mwezi Desemba mwaka 2016.

Imeshuhudiwa hivi karibuni msururu wa manguli mbalimbali wa Hip Hop wakifunga ndoa na wapenzi wao, ambapo msanii wa mwisho hivi karibuni ni Fid Q ambaye ameungana na Mwana FA, AY.