H Baba aanika ukweli kuhusu ndoa yake

Ijumaa , 5th Apr , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Hamisi Ramadhani maarufu kama H Baba, amezungumzia suala la kutalikiana na mkewe Flora Mvungi, na kusema kwamba hajamtaliki mkewe kama inavyodaiwa.

Akizungumza na www.eatv.tv, H Baba amesema kwamba kitu anachojua ni kwamba Flora bado ni mkewe kwani yeye ndiye aliyeoa, hivyo kama ni talaka yeye ndiye mwenye kuitoa lakini kamwe hajafanya hivyo.

H Baba ameendelea kusema kwamba kauli ya Flora kuwa ndoa ya wawili hao imekufa sio kweli, na kama Flora ndiye aliyeoa basi atoe talaka ili kuvunja ndoa hiyo.

H Baba akifunguka zaidi 

 

“Maisha yangu ya muziki hayaingiliani na familia yangu na watoto, sikumuoa instagram, kwa sababu unapozungumza ili watu wakusikie, ili u-trend sio kitu cha busara kwa sababu unaongea uongo, mimi ninachojiua ni mtu ambaye sijampa talaka, na mtu ambaye hatuna ugomvi, mimi niko busy na baishara zangu".

“Kwa mfano mimi ningekuwa nimefungwa miaka mitano angeniacha!?. Na yeye ni mke wangu, mimi nimemuoa kwa dini na sheria za Kiislam, kwa hiyo kama ataomba talaka atanitafutia mke, atanitolea mahali atanipa huyo mke nitatoa talaka, mimi ninachojua yeye ni mke wangu. Wanaosema nan'gang'ania, mwanaume anang'ang'ania ndoa!?. Mimi naangalia watoto wangu, lakini hajaniomba na tupo vizuri, yule ni mke na atabakia kuwa mke”, amesema H Baba.

Hivi karibuni kumekuwa na mvutano kati ya wawili hao kudai kuwa wameachana. Taarifa ambayo imetolewa na mwenyewe mke wa H Baba, Flora Mvungi huku H Baba akiendelea kukanusha kuwa hajamtaliki mkewe na bado wako vizuri.

H Baba akiwa na mkewe na wasimamizi wao siku ya harusi