Harmonize ayaweka wazi mahusiano ya Lulu Diva, TID

Jumatatu , 30th Mar , 2020

Msanii Harmonize amethibitisha kuyaweka hadharani mahusiano ya Lulu Diva na TID, baada ya kupost kipande kifupi cha video wakiwa pamoja.

Kushoto ni Harmonize, kulia ni TID akiwa na Lulu Diva

Katika video hiyo aliyopost  Harmonize katika akaunti yake ya mtandao wa Instagram, imewaonyesha wawili hao wakijirekodi wimbo  wake wa "Bedroom" kisha akaandika,

"Mahusiano pendwa kwa sasa washaanza kufanana, mapenzi ni matamu mnapokuwa kitandani"

Ikumbukwe wawili hao wamekuwa karibu siku za hivi karibuni na kuonekana wakiwa pamoja sehemu mbalimbali lakini wamekuwa wakikana kama wapo mahusiano.

Hii hapa ni kauli ya mwisho aliyoitoa Lulu Diva alipoulizwa na EATV & EA Radio Digital kuhusu mahusiano yake na TID,   "Sina mahusiano na mtu yeyote nipo single, TID ni kaka yangu ila tupo karibu kwa sababu tumefanya kazi halafu pia nina ushkaji na wasanii wengi wa kiume"