Hatma ya Lulu kujulikana leo

Monday , 13th Nov , 2017

Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  leo Novemba 13 inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili muigizaji Elizabeth Michael (Lulu).

Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa tena Oktoba 19 mwaka huu, ilianza kwa kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili za mashtaka na mshtakiwa, na kisha kusikiliza maoni ya wazee wa baraza la mahakama na hatimaye mahakama kumkuta Elizabeth na hatia ya kuua bila kukusudia.

Elizabeth Michael anatuhumiwa kumuua bila kukusudia aliyekuwa  mpenzi wake na muigizaji mwenzake,  Steven Charles Kanumba, mnamo April 7, 2014.