Hatma ya ndoa ya Irene Uwoya kujulikana

Jumamosi , 26th Oct , 2019

Baada ya kuwa na kitendawili alichokuwa anakiweka Irene Uwoya kupitia mtandao wa Instagram inayosema kuhusu tarehe 26 Oktoba, sasa imejulikana kuwa ni ndoa kutokana na tetesi zinazoendelea katika mitandao ya kijamii.

Irene Uwoya na anayedaiwa kufunga naye ndoa

Muda mchache uliopita katika mtandao wa Instagram, baadhi ya mastaa waliposti picha ya Irene Uwoya na mwanaume mmoja wakiwa wamevalia mavazi yanayomaanisha wanafunga ndoa yaani 'suti na shela'.

Mastaa walioandika ni pamoja na Irene Paul, ambaye amesema, "sijaalikwa na kadi sijapewa, naelewa kiutu uzima lakini Irene Uwoya nakutakia mafanikio mema mama, kapanga Mungu , sijashuhudia lakini picha naiona sasa mimi nani kupinga?. Bado tunataka kujua leo ni 'after party' ya ndoa, ni kuringishiwa cheti au hiyo suti na sura? au ni dinner au ni nini kukoma leo tutakoma 26.10, i saved the date". 

Naye muigizaji Duma ameandika, "hongera sana mama Irene Uwoya" .

Alipotafutwa mmoja ya watu wake wa karibu, akasema kuwa masuala yote yanayoulizwa na kuzunguka vichwani mwa watu yatajulikana hii leo kwenye hafla maalumu ambayo Irene Uwoya ameiandaa.

Siku ya leo, Irene Uwoya amealika vyombo vya habari, mastaa na baadhi ya watu kuhudhuria katika hafla yake itakayofanyika katika moja ya hotel iliyopo Posta Jijini Dar es Salaam.