Kesi ya Wema Sepetu bado ngumu

Wednesday , 13th Sep , 2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam inatarajia kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji nyumbani kwa Wema Sepetu ifikapo Oktoba 4, 2017.

Msanii wa filamu Wema Sepetu

Hatua hiyo inatokana na kuwasilishwa kwa pingamizi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kutoka kwa wakili wa utetezi , Peter Kibatala, kwamba kielelezo hicho kina mapungufu ya kisheria, hivyo kisipokelewe.

Kutokana na maelezo hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 4, 2017 kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Wema Sepetu anashtakiwa kwa kosa la kukutwa na msokoto wa bangi pamoja na karatasi maalum za kuvutia dawa hiyo baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake.