Alhamisi , 22nd Mar , 2018

Mkongwe wa muziki wa Taarab nchini Khadija Kopa amedai kwamba hata ikitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo kikimpa nafasi ya kuwa Mbunge kupitia chama chao hawezi kukubali na anaamini pia hawawezi kumpatia.

Khadija Kopa amesema anaamini CHADEMA haiwezi kumpa yeye nafasi ya uongozi kwa kuwa wanamjua vilivyoj jinsi alivyo CCM kindaki ndaki.

Aidha ameongeza kwamba "Kwani hawana  demokrasia mpaka wanipe mimi? Kwani wanapeana peana tu. Akhaa najua hawawezi kunipa eti".

Mbali na hilo mkongwe huyo amedai hajawahi kufikiria kwenda chama cha upinzani kwani hajaona pa kwenda.
Akiizungumzia CHADEMA, Bi. Khadija amesema hakifahamu chama hicho zaidi ya kulisikia jina na bendera.