Ijumaa , 18th Mei , 2018

Msanii Alikiba kwa mara ya kwanza amezungumzia asili ya jina lake Ali Kiba, ambalo wengi wanaamini ndiyo jina lake halisi, jambo ambalo halina ukweli hata chembe.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Alikiba amesema jina la Alikiba sio jina lake halisi bali ni jina la utani, ambalo alipewa kabla hajazaliwa.

Akifafanua chanzo cha jina la Kiba, Alikiba amesema wakati mama yake ana ujauzito wake ndugu na marafiki zake walikuwa anampenda kumbana nguo zake na vibanio, wakawa wanamtania mama vibanio mpaka alipozaliwa akaitwa jina hilo la utani, na ndipo lilipozaliwa jina la kiba.

“Kiba ni jina langu mimi tena la utani, wakati mama yamgu alipokuwa na ujauzito wangu, sasa wale mawifi zake, marafiki walikuwa wanambana nguo kwa vibanio wakawa wanamtania mama kibanio, mpaka nilipozaliwa wakawa naniita kibanio, ndio lilipozaliwa la 'Kiba', jina langu halisi mimi ni Ali Saleh Gentamilan", amesema Alikiba.

Jina la 'Kiba' limekuwa kubwa kiasi kwamba karibia watu wote kwenye familia yao wanalitumia akiwemo mdogo wake Abdu Kiba, dada yake Zabibu Kiba na mtoto wake Kiba Junior.