Jumapili , 1st Mar , 2015

Msanii wa muziki Hisia amepata shavu la kuutangaza muziki wake na Tanzania kwa ujumla, akiwa star wa kwanza kutoka Tanzania kupata shavu la kuwafikia mashabiki kwa sanaa yake kupitia mtandao wa Yahoo.

Hisia

Hatua hii itawawezesha wapenzi wa muziki hususan wale wa kutoka nje ya nchi kuufikia muziki wake kwa njia hiyo ya kisasa zaidi, hii ikiwa ni ishara ya hatua nyingine kubwa ya msanii na sanaa kutoka hapa Tanzania ambapo hapa tumeweza kupiga story na Hisia juu ya nafasi hii.