Ijumaa , 27th Mar , 2020

Mtangazaji wa kipindi cha 5 Selekt ya EATV, T Bway 360, amesema ni kweli anapenda sana sterehe pia ametoa onyo kwa wale wote wanaommendea mpenzi wake Kim Nana.

Akiiambia EATV & EA Radio Digital , kuhusu kupenda starehe na kula bata amesema anautumia vizuri muda wa ujana wake kwa sababu hata akizeeka asijutie kile alichokifanya enzi za ujana.

"Ni kweli napenda kuishi maisha ya starehe kwa sababu maisha yanakwenda kasi sana hapo kuna uzee na ujana unapita, kwa nini nisiishi maisha ya ku-enjoy ili nijivunie kuishi hivyo, siyo baadaye nikizeeka niyatamani tena, mimi ni mtu wa bata, nakula bata na hata kazi yangu inauhusiano na bata" amesema T Bway

Pia T Bway amezungumzia ishu ya kutoa onyo kwa  watu wanaommendea mpenzi wake Kim Nana ambaye ni mzazi mwenziye kwa sasa ambapo amesema   "Huwa nashikaga simu yake kuna muda hata yeye ananiambia kuna mtu flani kama  amemfuata DM anamtaka, ninachotaka kuwaambia wajue tu kwamba sasa hivi ni mzazi, ana mtoto na mimi na analea