Jumanne , 8th Oct , 2019

Mchekeshaji maarufu Bongo Idris Sultan, amejibu madai ya kutafutiwa wanawake na msanii wa kike Lulu Diva , pamoja na matumizi ya condom anapokutana kimwili na mpenzi wake.

Idris Sultan

Kama unakumbuka siku kadhaa zilizopita tulikuwekea stori ya Lulu Diva ambaye alisema anamtafutiaga Wanawake Idris Sultan kwa kumpatia namba za simu kisha anamalizana nao kwa shughuli zake binafsi.

Sasa kuhusu suala hilo, EATV & EA Radio Digital, imempata Idris Sultan ambaye amekiri 'issue' hiyo pia amefunguka kuhusu mpenzi wake Lulu Diva.

"Ndiyo ananipa sasa kwanini nidanganye ila hata sikumbuki namba ngapi amenipa ila nikimuona akiwa na Mwanamke huwa namuuliza huyu ni nani kisha namwambia nataka nifanye nae kazi, ila shemeji yangu kwa Lulu Diva namjua na nilishawahi kuongea naye kwenye simu ila anapenda mambo ya siri sana", ameeleza.

Aidha kwa upande wa matumizi ya kinga wakati anafanya mapenzi Idris Sultani amesema kila siku huwa anatumia condom pia yupo salama sana.