Jumamosi , 30th Nov , 2019

Mchekeshaji na Muigizaji Idris Sultan amesema rapa Billanass amuombe sana Mungu yasimkute matatizo kama ambavyo yalimkuta yeye ya kuitwa Kituo cha Polisi maana atapata tabu sana.

Kushoto pichani ni Idris Sultan na upande wa kulia ni Billnass

Idris Sultan amefunguka hayo mara baada ya Billnass kumletea utani kwenye suala la u-serious, ambalo lilimkuta Idris Sultan kwa kuitwa polisi na kuwekwa ndani kwa siku kadhaa kwa kosa la kutumia Kompyuta kwa kuichapisha picha yake na Rais Magufuli.

Akieleza EATV & EA Radio Digital, Idris Sultan amesema Billnass amuombe mungu yasimkabili matatizo maana akianza kumuandika hata TID hataweza kumuokoa.

"Watu walihitaji kufurahi na wanahaki ya kufurahi, naamini hata Billnass hana nia mbaya na mimi sidhani kama amefurahia kweli ila anajua haya mambo yanatokea na yatakwisha, vyote kwa vyote ni utani tu na mtu yeyote anaweza akafanyiwa na hata nikishikiliwa tena sitegemei watu walie au wahuzunike" amesema Idris Sultan