Imefichuka: Amber Ruty amechepuka kwenye ndoa yake

Jumapili , 10th Feb , 2019

Imebainika kwamba ndoa mpya kati ya video vixen, Amber Ruty na mume wake Said, iliingia kidudu mtu baada ya mwanaume mmoja kujitokeza na kusema kwamba amewahi kukutana kimwili na mwanadada huyo, ikiwa ni miezi miwili tu imepita tangu afunge ndoa.

Siri hiyo imewekwa wazi kwenye FNL ya East Africa Television, baada ya kijana aliyejitambulisha kwa jina la Silas, kukiri kuwa amewahi kufanya mapenzi na Amber Ruty hivi karibuni.

Silas amesema taarifa hizo ni za ukweli na wala sio kiki, licha ya kwamba ukweli wake umemletea matatizo makubwa ikiwemo kupigwa na Amber Ruty mbele za watu.

Itazame hapa