Jumatano , 29th Jan , 2020

Mkali wa RnB Bongo, Ben Pol amefunguka na kusema moja ya sababu inayofanya watu kuzungumzia sana penzi lake ni kutokana na kuwa na mwanamke mzuri ambaye amebadilisha maisha yake kwa sasa.

Pichani Ben Pol na mpenzi wake Anerlisa Muigai

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya cha SalamaNa, ambacho kitaruka kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku, Ben Pol amesema kuzungumziwa kwake inatokana na mpenzi wake kuwa mzuri.

"Kwanza nadhani watu hawajanizoea kwa kuweka mahusiano yangu hadharani, kwahiyo imeleta mitazamo tofauti, pili mpenzi wangu anaongelewa kiupande wake kwa kule kwao na hata huku kuna Watanzania ambao walikuwa wanamfuatilia kwa muda mrefu, halafu ni mtu maarufu  na kitu kingine ni mzuri" ameeleza Ben Pol.

Aidha msanii huyo akizungumzia juu ya kubadilishwa maisha yake na mpenzi wake raia wa Kenya Anerlisa Muigai, amesema, "Ameniweka karibu na Mungu zaidi, ameniongezea utu na ubinadamu wa kawaida, ananisaidia katika mawazo ya kazi, ana sikio zuri la muziki, jicho la fashion, na tunasaidiana kwenye kazi zetu".