Jumamosi , 7th Dec , 2019

Msanii na video vixen Bongo Amber Rutty, ametangaza kutokuwa kwenye mahusiano tena, sasa hivi yupo "single",  na ameachana na aliyekuwa mpenzi wake aitwaye Said Bakary.

Picha ya Amber Rutty akiwa na aliyekuwa Mume wake

Amber Rutty ametangaza hivyo kupitia "Status" za mtandao wa kijamii wa WhatsApp na Instagram ambapo ameandika,

"Hongera zao walio olewa jamani duuh, kama ndoa zenyewe ndiyo hivi nimeshindwa, kumbe wanaodanga wanajua wanachokifanya kina maana gani loh, ebu nipumue zangu na mimi nipate danga jipya mjino, Mungu atanionyesha  njia sahihi Inshalaah" ameandika Amber Rutty.

Wawili hao walikuwa kwenye ndoa kwa Mwaka mmoja na walianza mahusiano yao miaka 6 iliyopita.

Mara ya mwisho kufanya mahojiano na EATV & EA Radio Digital waliahidi kama hawataachana na walisema bado wanaendelea kumtafuta mtu ambaye aliyevujisha video zao zilizokosa maadili, ambazo ziliwafanya kuwekwa ndani na kupandishwa mahakamani.