Juma Sharobaro aeleza anavyosumbuliwa na kinadada

Jumamosi , 2nd Nov , 2019

Msanii kutoka nchini China anayefanya shughuli zake nchini Tanzania, Juma Sharobaro, amedai kuwa huwa anasumbuliwa sana na "message" kutoka kwa wadada wanaomtongoza kupitia mitandao ya kijamii.

Juma Sharobaro

Juma Sharobaro ameileza EATV & EA Radio Digital kuwa anatumiwa message nyingi za kinadada hasa katika mtandao wa kijamii wa Instagram lakini kutokana na utamaduni wa Kichina, anatakiwa awe na mwanamke mmoja tu ambaye tayari anaye.

"Watu wengi wananitumia message, nafikiri kufuatana na utamaduni wa China inabidi nishikilie mtu mmoja tu kwa hiyo siwezi kuwa na moyo wa kutafuta mchepuko. Huwa wananitafuta ila siwajibu za Instagram ndiyo nyingi zaidi na kuhusu mastaa hiyo ni siri kidogo", ameeleza Juma Sharobaro.

Pia ameendelea kusema bado hajafikiria kuwa na mpenzi Tanzania kwa sababu ana mchumba wake  ambaye ni raia wa China na anamtembelea mara kwa mara, japokuwa anaishi kwao China.