Kabula afichwa

Wednesday , 13th Sep , 2017

Muigizaji maarufu wa filamu Tanzania Miriam Jorwa maarufu kwa jina la Jini Kabula, ameruhusiwa kutoka hospitali ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa na kupelekwa kusikojulikana.

Mwandishi wa East Africa Television alifanya mahojiano na mtu wa karibu wa msanii huyo na kusema Kabula alisharuhusiwa kutoka hospitali alikokuwa akitibiwa matatizo ya akili, na kwa sasa amepelekwa mahali ambako ndugu wa karibu hawakutaka pajulikane kwa watu, ili kumuweka mbali na watu kuweza kumsaidia kutulia.

"Kabula alishatoka kitambo sana, siku zile zile hakukaa sana, lakini hayuko Dar es Salaam ndugu zake hawataki ijulikane, muache apumzike", alisema mtu huyo wa Karibu na Kabula

Kabula alipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na matatizo ya akili ambayo yalimpata, ambapo daktari alisema yametokana na msongo wa mawazo.