Jumamosi , 25th Jan , 2020

Msanii wa BongoFleva Peter Msechu, ametangaza kufunga ndoa na  mpenzi wake wa muda mrefu aitwaye Ama Lauren, ambaye ni mzazi mwenziye siku ya leo Januari 25, 2020 kuanzia 8:30 mchana hadi 10:30 jioni, katika kanisa la KKKT ushirika wa Ununio.

Kushoto pichani ni Peter Msechu, kulia ni Baba Levo

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital Peter Msechu, amesema mkewe huyo mtarajiwa alianza naye mahusiano miaka 12 iliyopita, na mtu wa suprise wa harusi yao akiwa Baba Levo  basi itakuwa imefia hapo.

"Ni kweli nafunga ndoa leo, sasa hivi tupo kanisa la KKKT Ushirika la Ununio kuanzia 8:30 mchana hadi 10:30, baada ya hapo ukumbi utakuwepo maeneo ya Mbezi Beach kuanzia 12:00 jioni hadi usiku mwingi, tulianza mahusiano siku nyingi sana kama miaka 12 iliyopita na tumebahitika kupata watoto wawili" ameeleza Peter Msechu.

Aidha ameendelea kusema "Suprise zitakuwa nyingi  watu wataona tu ukisema kama atakuwa Baba Levo hata hiyo suprise yenyewe itakuwa imeshakufa, watu wengi wamealikwa, halafu ndoa ni siri haiwezi kuwa kama matangazo ya vifo ila waelewe naingia katika hatua mpya namshukuru Mungu" ameongeza.