Alhamisi , 21st Mar , 2019

Msanii wa Bongofleva na aliyekuwa mshindi wa shindano la BSS mwaka 2015, Kanyumba, amekataa  kuongelea taarifa zilizotufikia kwamba ana mtoto ambaye amemtelekeza na hataki jamii ifahamu kwamba alipata mtoto.

Kayumba

Siyo hali ya kawaida kwa mzazi kuacha kumuongelea mtoto wake kama hakuna tatizo, na habari ilizonazo eNewz ni kwamba msanii huyo amemkimbia mtoto na kususa malezi kwa kile alichodai kwamba muziki bado haumlipi, hata hivyo Kayumba aligoma kabisa kuongelea tuhuma hizo na kusema hawezi jibu kitu chochote kwa wakati huu.

"Sidhani kama kuna umuhimu wowote wa mashabiki kujua maisha yangu, binafsi ninachofahamu ni kwamba mashabiki zangu wanapaswa kupata muziki mzuri kutoka kwangu ila mambo ya familia sio vyema wao kuyafahamu kwanza yanaweza yakawafanya wakaacha kufuatilia muziki wangu kwa kuwa hawajawahi kusikia nikizungumzia maisha yangu binafsi tangu wamenifahamu. Aliongea Kayumba.

Hata hivyo Kayumba alisema kwa sasa anahitaji sapoti ya mashabiki zake katika muziki wake kwa kuwa bila wao yeye hawezi kufanya chochote na amewaambia wategemee mambo mazuri kutoka kwake kwa upande wa muziki ila kwa sasa kuna video yake mpya ambao amefanya na Director Snaipa.