Jumamosi , 21st Jul , 2018

Msanii wa Bongo Fleva Feza Kessy amefunguka kuwa wanaume wengi anaoingia nao kwenye mahusiano wanapenda cheko lake.

Msanii wa Bongo Fleva Feza Kessy.

Feza amefafanua kuwa hata yeye alikuwa hajui kama anacheka vizuri kiasi cha kufanya wanaume kupagawa juu ya cheko hilo

Akizungumza na www.eatv.tv Feza amesema, amegundua hilo baada ya kukutana na maoni mengi kuhusu cheko lake, pia wanaume wengi anaokutana nao kitu cha kwanza kukisifia juu yake ni kicheko.

Mwanzo nilikuwa najua watu wananitania tu, ila bwana kila mwanaume nayempata unakuta anapenda cheko langu lakini mwanzo ilikuwa ngumu kuamini kuwa wanaume wengi wanapenda kicheko changu, lakini kwa sasa hivi naamini hata mpenzi wangu ndio kitu kikubwa anapenda”,amesema Feza kessy.

Lakini Feza ameingiwa na hofu kwa kusema kuwa muda mwingine hafurahii kuona wanaume wengi wanampendea hicho kitu na anaogopa siku akiwa hana hicho kicheko itakuwa rahisi kuachika.