Ijumaa , 18th Sep , 2020

Msanii wa HipHop hapa nchini Tanzania Dogo Janja amefunguka kuwa alijaribu kuvuta bangi kwa mara ya kwanza ila kilichomtokea ni kuchekacheka kila wakati hivyo akaona haimkubali na kuamua kuachana nayo.

Msanii Dogo Janja kwenye show ya SalamaNa

Dogo Janja ameeleza hilo kwenye show ya SalamaNa ya East Africa TV ambayo inayorushwa kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku, ambapo aliulizwa kama aliwahi kujaribu kuvuta bangi.

"Mimi sivuti bangi, ningetaka kuvuta ningefanya tangu zamani kwa sababu nilikulia mazingira ya hivyo na niliona madhara yake, nilijaribu mara moja nikawa nacheka tu nikaona hainikubali"

Aidha Dogo Janja ameongeza kuwa  "Nisingekuwa mwanamuziki basi ningekuwa Mwakinyo fulani hivi au ningekuwa muhuni ambaye ningekuwa nimeshafukiwa, lakini sasa hivi nikiwa Arusha huwa nawatuliza vijana wenzangu wanaopanga uhuni"