Kilichomukoa Blue baada ya kutaka kuchanganyikiwa

Jumanne , 11th Aug , 2020

Mkali wa hizi kazi Byser Babilone Mr Blue amesema amepitia wakati mgumu hadi kutaka kuchanganyikiwa na kuacha muziki kipindi ambacho mama yake mzazi alipofariki dunia miaka kadhaa iliyopita.

Msanii wa HipHop Bongo Mr Blue

Mr Blue amesema sasa hivi anajiona kama nyani mzee kwa sababu mama yake na ndugu wengi wa mama yake mzazi wametangulia mbele yaki na hata baba yake pia ametangulia kipindi yeye ana umri mdogo sana.

Aidha ameongeza kusema alivyokutana na hali hiyo alitaka kuchanganyikiwa na ilifika hatua alifikiria kuacha muziki, ila anamshukuru mkewe na mama watoto wake Wahda ambaye amemfanya kusahau hayo yote.

Ikumbukwe Mr Blue amewahi kusema mkewe Wahda anampenda sana kwa sababu amemvumilia wakati msanii huyo alipokuwa na wanawake wengine watatu ndipo alipoamua kumchagua yeye