Kinachomchukiza Matumaini kwa Ebitoke

Jumatano , 12th Feb , 2020

Mchekeshaji wa muda mrefu hapa nchini Matumaini, amesema anamkubali sana mchekeshaji wa sasa Ebitoke ila anachukizwa na suala lake la kupenda skendo, kashfa na kiki anazofanya kwa hivi sasa.

Picha ya wachekeshaji kushoto ni Matumaini, kulia Ebitoke

Matumaini amesema hayo wakati anapiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni.

"Mimi nimekaa Kaole miaka minne bila ya kuchaguliwa kufanya maigizo, siku ambayo naambiwa nikarekodi kipande cha kuigiza na Ray nilitoka kwa mguu kutoka Yombo hadi Kimara Suka sehemu ambayo alikuwa anarekodi, kwa sasa hivi nampenda sana Ebitoke kwenye suala la uchekeshaji na anaweza sana ila shida yake ana skendo chafu" amesema Matumaini.

Pia Matumaini amezungumzia kuhusu uhusiano wake na mchekeshaji mwenziye ambaye ni Kiwewe baada ya taarifa za wao kuwa kwenye mahusiano.

"Kiwewe ndiyo aliona kipaji changu tangu mwaka 2005 ndipo tukaanza kuwa marafiki, na muunganiko wetu ulikuja baada ya kufanya mazoezi pamoja ila hatupo kwenye mahusiano ni marafiki tu ila unaweza ukasema ni wapenzi" ameongeza.